Posts

Showing posts from 2021

WANAVYUO KUWENI NA MALENGO

"WANAFUNZI NA WAENDESHAJI VYUO VIKUU JIWEKEENI MALENGO MAKUBWA" Alhaj Dr. Mangochi Wanafunzi wa vyuo vikuu,  wahitimu waendeshaji na wamiliki wa vyuo vikuu pamoja na wadau wote wa elimu nchini wametakiwa kuwa na malengo makubwa ili kufikia hatua iliyofikia na nchi nyingine. Akiongea kwenye mahafali ya chuo cha utumishi na chuo kikuu cha Sauti jana mjini Mtwara mkuu wa chuo kikuu cha Mar-wa Dr. Nurdin Mangochi amesema dunia imefika mbali sana na malengo yetu yakiwa madogomadogo dunia inazidi kwenda mbali na kupiga hatua kubwa zaidi huku ikituacha sisi tukiendelea kuwa watazamaji na watumiaji. "Wakati nchi sasa zinadhamira ya kufundisha watu wote kwa kiwaango cha chuo kikuu na kuwa na taasisi nyingi na kufundisha fani zote na kubuni fani nyingi mpya bado sisi tuna vyuo vichache,  tunatoa mafunzo kwenye vitivo vichache na wanafunzi wachache zaidi pia tunatumia mbinu za miaka hamsini nyuma." Amesemaa na kuendelea "bado jamii inaona haiwezi kuanzisha vyuo vikuu kila...

STOP SHARING

*NOTE* Stop  forwarding  as received  without proper  Verification because you might put someone's life in danger. *There is no free Money,* There is no free Credit There is no free Data anywhere  in  Africa  via  Links Nadhan mnajua utofauti wa http na https What is the difference between *http* and *https*? Please make sure you read this to the end. Some of you may be aware of this difference, but it is worth sharing for many that are not. The *main* difference between *http://* and *https://* is all about keeping you *secure*.  *HTTP* stands for *Hyper Text Transfer Protocol*.  The *S* stands for *"Secure"*.  If you visit a Website or web page, and  *PLEASE* look at the address in the web browser and  *IF* it begins with the following: *http://*.  This means that the website is talking to your browser using  the regular unsecured language. In other words, it is possible for someone to "eavesdrop" on your compu...

MISINGI YA KUISHI PAMOJA

*Misingi ya kuishi Pamoja!* . 1. Ukifika Sehemu... *Salimia* 2. Ukiondoka Sehemu..... *Aga* 3. Ukisaidiwa....... *Shukuru* 4. Ukiahidi...... *Tekeleza* 5. Ukikosea.... *Omba Msamaha* 6. Kama Hujaelewa..... *Uliza* 7. Unacho... *Gawa Kwa Wengine* 8. Huna.... *Usione Donge* 9. Ukivunja.... *Lipa* 10. Kama Hupendi...... *Heshimu* 11. Ukipendwa... *Onesha Upendo* 12. Huwezi Kusaidia... *Usisumbue* 13. Ukiharibu... *Rekebisha* 14. Ukikopa.... *Lipa* 15. Wakikuuliza .... *Jibu* 16. Ukiwasha....... *Zima* 17. Ukifungua...... *Funga* 18. Ukinunua.... *Lipa* 19. Ukichafua.. *Safisha* 20. Ukipungiwa..... *Punga* 21. Ukipewa.... *Shukuru* 22. Ukiazima... *Rudisha* *''Ukizifuata kanuni Hizi, Utaona Jinsi Utakavyoishi Na Watu Vizuri Hata Kama Huna Hela, Hii Ni kwa Binadamu Wote Hata Kama Ni Kiongozi'''*

ITIFAKI IMEZINGATIWA

ITIFAKI IMEZINGATIWA! NDIYO KITU GANI HASA? Jumamosi tarehe 26 Juni, 2021. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Ijumaa  tarehe 25 Juni, 2021 alikutana na Maaskofu wa Kanisa Katoliki katika Ukumbi wa  Makao Makuu ya Baraza la Maaskofu Wakatoliki (TEC) Kurasini  Dar es Salaam na kuhutubia taifa kutokea hapo. Nilipata bahati ya kufuatilia mkutano ule na miongoni mwa mambo ambayo yalikamata kichwa changu ni hili neno "ITIFAKI IMEZINGATIWA." Nimekuwa nikijiuliza mara kwa mara, ni nini hasa? Lina maana gani hasa? Nilichobaini katika mkutano ule ni kwamba, tukiacha Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye itifaki ni sehemu ya maisha yake, mtu mwingine pekee anayeifahamu itifaki vilivyo ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mbeya ambaye ni Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Askofu Gervas Nyaisonga. Baba Askofu Nyaisonga anaijua itifaki ya Kanisa Katoliki na ya nchi mpaka unasikia raha kumsikiliza. Wengine wote waliobaki niseme...

KEF HAKUNA KUFELI RURAL INITIATIVE - SUCCESS LEVEL

*KEF HAKUNA KUFELI RURAL INITIATIVE - SUCCESS LEVEL*  KALAMU EDUCATION FOUNDATION *(KEF)* tumeandaa Semina maalumu kwa wahitimu wa KIDATO CHA SITA 2021 katika Wilaya Tufanyazo Juhudi Ili Kuendeleza Juhudi na Athari za Matokeo Chanya ya Program zetu za Hakuna Kufeli Rural Initiative Maeneo Husika.  *AWAMU YA KWANZA KIBITI - PWANI.*   *SIKU* : KESHO 22-05-2021  *MUDA*: SAA 2:00 Asubuhi hadi SAA 10:30 Alasiri  *AGENDA:-* 📈🗒️  *1* . KUFAHAMU TARATIBU ZA MAOMBI VYUO KUPITIA TCU NA BODI YA MIKOPO.  *2* . MUONGOZO WA KUUTUMIA VYEMA MUDA WA KUSUBIRI MATOKEO NA ELIMU YA JUU.  *MAHALI*:- KIBITI - BUNGU,  KEF -  RESOURCE CENTER, KINYAMALE VILLAGE  *WALENGWA* : Wahitimu wote Wenyeji wa MKURANGA, KIBITI & RUFIJI.  *MAWASILIANO* Mwl Sued 0784222146  *VIJANA WETU, HAZINA YETU.* KARIBUNI

IPO SIKU

Image
IPO SIKU Ipo siku ,Allah alonipangia Ipo siku, ya kwangu  itafikia Ipo siku ,Na Mimi ntatulia Ipo siku Ipo siku ,Mitihani itaisha Ipo siku,Ntaenjoy maisha Ipo siku ,Yataisha yakuchosha Ipo siku Ipo siku ,Na Mimi ntaolewa Ipo siku,Mahari ntatolewa, Ipo siku,uwezo wake moliwa Ipo siku Ipo siku ,Nami ntaitwa mke Ipo siku ,Ntakuwa mke wake Ipo siku,Na mimi nistirike  Ipo siku Ipo siku ,Duniani taondoka Ipo siku ,Taitika kwa RABUKA ipo siku,nanyi mtanikumbuka Ipo siku Ipo siku ,Naamini itakuja Ipo siku ,Na Mimi ninaingoja Ipo siku,Ya kwake mola mmja IPO siku Mtunzi BINT SKAZWE Contact, 0673178456

UMUHIMU WA KUTUNZA MUDA

Image
*UMUHIMU WA KUTUNZA MUDA* Na SS Nyakubandya Ni kawaida ya mswahili kusikia akisema *"napoteza poteza muda*". Wachina wanamsemo:"inch ya muda ni sawa na inch ya dhahabu lakini huwezi kununua inch ya muda kwa inch ya dhahabu" Muda ni mfinyu sana na kila jambo limeegemezwa katika muda, matumizi yako mazuri ya muda yatakufanya upate unachokitaka katika hii dunia na kesho akhera.Ikiwa siku moja ina masaa 24, swali ni je haya masaa 24 unayatumiaje? Wote waliofanikiwa wametumia masaa haya haya 24 ambayo kila mtu anayo. Kwa bahati mbaya muda unasifa ambazo hakuna mtu angependa kuzisikia; muda uko kasi sana kuliko chochote, muda ndiyo kitu pekee ambacho hakiwezi kufidiwa katika maisha lakini pia ndio kitu pekee kisichoweza kusimama.(Tizama masaa yako na mambo unayoyafanya ndani ya saa 24) Mambo yanayopoteza muda ni mengi sana ila hapa nitataja machache ikiwemo kutizama *mpira* (mashabiki naomba mnisamehe hapa maana najua hamtaki kusikia jambo hili) ndani ya lisaa...

OPEN YOUTH DIALOGUE - TIMUN 2021

Image

WAJUE WASHINDI 10 WA MASHINDANO YA QUR AN KWA WANAFUNZI WA SHULE ZA SEKONDARI MANISPAA YA BUKOBA

Image
*MASHINDANO YALIYOANDALIWA NA TAMSYA MANISPAA YA BUKOBA NA KUFANYIKA KATIKA MSIKITI WA JAMIA - BUKOBA MANISPAA TARAHE 08.05.2021* *NO.1* FATUMA MOHAMED - NYANSHENYE SEKONDARI  *NO.2*  SHAKIRA ISMAIL - NYANSHENYE SEKONDARI   *NO.3* HAWA ABBAS - KEMONDO SEKONDARI  *NO.4* HAMIMU DAUDA - BUKOBA SEKONDARI  *NO.5* MUZDALIFA RAJAB - NYANSHENYE SEKONDARI  *NO.6* NASRIN AHMED - HAMGEMBE SEKONDARI   *NO.7* HASHIRU SIRAJI - NYANSHENYE SEKONDARI   *NO.8* MANSURA MUSSA - NSHAMBYA SEKONDARI   *NO.9* AZAYYA IS-HAQ - NYANSHENYE SEKONDARI  *NO.10* YUSUPH ABUBAKAR NYANSHENYE SEKONDARI

BURIANI BALOZI ABBAS KLEIST SYKES

Image
Mwezi October 1999 nilikuwa Dubai na nikikaa Carlton Hotel. Siku moja jioni simu yangu ikalia. Walikuwa BBC London Idhaa ya Kiswahili wanataka kunihoji kuhusu Mwalimu Julius Nyerere ambae wakati ule alikuwa amelazwa St. Thomas Hospital, London. Ulikuwa mwaka wa pili toka kitabu changu, ‘’The Life and Times of Abdulwaid Sykes (1924- 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Aganst British Colonialism in Tanganyika,’’ kichapwe na kitabu hiki kikawa kimenifanya nifahamike na sababu kubwa ni kuwa kilikuja na historia mpya ya yeye Mwalimu Nyerere mwenyewe, historia ya TANU na historia nzima ya kudai uhuru wa Tanganyika. Kitabu kilimweeleza Mwalimu Nyerere kwa namna ambayo hakuna mwandishi alipatapo kufanya hivyo. Hii nadhani ndiyo ikawa sababu ya BBC kutaka kunisikia nikimzungumza Mwalimu Nyerere. BBC wakawa wanataka tuzungumze kidogo kuhusu Mwalimu na jinsi Watanzania walivyoathirika na ile hali ya Mwalimu kuwa kwenye matibabu Uingereza. Katika kipindi kile cha maradhi ya M...

UJUE MGOGORO WA ARDHI KATI YA ISRAEL NA PALESTINA NA SULUHISHO LAKE

Image
Na Masudi Rugombana  Israel ni taifa pekee la kiyahudi Duniani. Taifa hili linapatikana Mashariki ya bahari ya Mediterrania, ni taifa dogo kwa eneo, likiwa na ukubwa wa kilomita za mraba 20,770. ( Imezidiwa ukubwa wa eneo na Wilaya ya Sikonge nchini Tanzania kwa tofauti ya kilomita za Mraba 7103 ). Israel inapakana na nchi za Syria na Lebanon kwa upande wa kaskazini, Jordan na eneo la Palestina la Ukingo wa Magharibi (West bank) kwa upande wa Mashariki na kusini inapakana na Misri na eneo la Palestina la Ukanda wa Gaza ( Gaza strip ).Taifa hili lina idadi ya watu Milion 8,680,000 kwa takwimu za mwaka 2017. Idadi ya Wayahudi ni Milioni 6,484,000 sawa na 74.7% (Idadi hii inajumuisha Walowezi wa Kiyahudi wanaoishi ukingo wa Magharibi (West bank) na eneo la Milima ya Golan). Waisrael Waarabu ni Milioni  1,808,000 sawa na  20.8% ya raia wote wa Israel. Idadi ya Wakristo ambao sio Waarabu pamoja na watu wa jamii ya bahai ni 388,000 sawa na 4.5% ya raia wote wa Israe...