WANAVYUO KUWENI NA MALENGO

"WANAFUNZI NA WAENDESHAJI VYUO VIKUU JIWEKEENI MALENGO MAKUBWA" Alhaj Dr. Mangochi

Wanafunzi wa vyuo vikuu,  wahitimu waendeshaji na wamiliki wa vyuo vikuu pamoja na wadau wote wa elimu nchini wametakiwa kuwa na malengo makubwa ili kufikia hatua iliyofikia na nchi nyingine.

Akiongea kwenye mahafali ya chuo cha utumishi na chuo kikuu cha Sauti jana mjini Mtwara mkuu wa chuo kikuu cha Mar-wa Dr. Nurdin Mangochi amesema dunia imefika mbali sana na malengo yetu yakiwa madogomadogo dunia inazidi kwenda mbali na kupiga hatua kubwa zaidi huku ikituacha sisi tukiendelea kuwa watazamaji na watumiaji.

"Wakati nchi sasa zinadhamira ya kufundisha watu wote kwa kiwaango cha chuo kikuu na kuwa na taasisi nyingi na kufundisha fani zote na kubuni fani nyingi mpya bado sisi tuna vyuo vichache,  tunatoa mafunzo kwenye vitivo vichache na wanafunzi wachache zaidi pia tunatumia mbinu za miaka hamsini nyuma."

Amesemaa na kuendelea "bado jamii inaona haiwezi kuanzisha vyuo vikuu kila mkoa na kila wilaya mpaka kwenye kata na bado kupata elimu ya juu inaonekana ni bahati kubwa. Hivyo vyuo vichache vilivyoko bado hatuviamini na kujiunga lazima mwanafunzi ahangaike sana ili kutimiza masharti magumu yaliyoko"

Amesema kuna vyuo duniani sasa vinatoa kozi zaidi ya elfu moja kwenye vitivo vingi na vitengo vingi kupita kiasi. Kwa sababu kila nyanja,  kila eneo na kila sekta inahitaji wataalamu wenye ujuzi stahiki. Zaidi ya hayo bado wanafunzi  humu nchini wanalazimika kusafiri mikoa na maeneo ya mbali ili kupata elimu ya juu. Wanafunzi wanapata usumbufu mkubwa

Dr. Mangochi amesema kwenye zama hizi nchi au jamii yoyote haiwezi kupiga hatua kwa kutegemea wataalamu wa kigeni. Amesema sekta ya uhandisi,  afya,  viwanda na TEHAMA  bado inategemea wataalamu kutoka nje na hata kwenye maeneo nyeti.

"Lazima tuwe na mikakati ya makusudi,  tuwe na mipango thabiti na malengo yetu yawe wazi ili sote tutekeleze huku tukiwa tumejiwekea muda wa kujitathmini. Mimi Naamini tunaweza"

Akasema na kumaliIa "Muhimu zaidi UDOM isishindane na MUM,  UDSM SAUTI au chuo kingine. Bali vyuo vyetu vyote kwa pamoja vijipime kwa kujilinganisha na vyuo vya nje. Vishindane na vyuo vya Kenya Afrika ya Kusini,  Misri,  China Japan na hata vyuo vya Ulaya"

Amesema mitaala na mfumo mzima wa masomo na uendeshaji ulenge kujenga ubunifu na kuondoa fikra ya kuajiriwa serikalini.

"Vyuo vitoe shahada za juu za ubunifu kwa vijana wengi,  aidha tuzalishe wahandisi wengi kila nyanja. Tutaweza kuanzisha viwanda na kupunguza fikra ya kuajiriwa. Pia sekta binafsi itaomarika. Serikali itakusanya kodi zaidi na itaongeza uwezo wa  kuajiri"
.....

Harith Nkussa
Mwandishi maalum wa mufti
Jumatatu 5.7.2021
Makorora. Tanga

Comments

Popular posts from this blog

SHULE ZENYE ADA KUBWA ZAIDI TANZANIA

STOP SHARING

RAFIKI WA KWELI