Posts

Showing posts from 2018

TANZANIA SHOTOKAN KARATE TOURNAMENT

Image
This year in Dar es salaam

NITAOA NIKIFIKA THELATHINI

NITAOA NIKIFIKA THELATHINI Si kama nataka kufa, kwa haya nitokwambia Ila nofia kujuta, pindi yakikutokea Nogopa  nafsi nisuta, mjomba nsipokwambia              Nitaoa nikifika thelathini Natambua nia yako, nia unopigania Sikukwacha peke yako, pekee kiteketea Shikamana na wenzako, usia me nakwambia               Nitaoa nikifika thelathini. Nataka kupa wosia, li kazi uufanyie Sio uje puuzia, sitajilaumu mie Kidogo hebu sikia, kisha ukazingatie             Nitaoa nikifika thelathini. Wangindo mi nawajua, na hasa nawatambua Kidogo kifanikiwa, haraka taka kuoa Mjomba we zingatia, usi harakie ndoa             Nitaoa nikifika thelathini. Kama ukipata kazi, tulia kwa kujipanga Usijivishe li vazi, kabla maisha kujenga Tena ipo wazi wazi, kuo...

RAFIKI WA KWELI

Image
Ni mida ya saa kumi na moja saa za jioni kijana anampigia simu rafiki yake na kusema "samahani rafiki yangu ninashida na hela, mama yangu anaumwa na hapa nilipo sina pesa ya matibabu. Rafiki anajibu "usijali!! Nipigie baada ya mechi saivi nipo kucheki game ya simba na yanga Baada ya mechi anampigia anakuta sim imezimwa Kama haamini hivi anapiga tena na tena  lakini bado simu haipatikani Anajaribu kuwatafuta marafiki zake wengine lakini wote wanasema hawana pesa. Mikono nyuma huku machozi yakimlenga anaamua kurudi hospitalini Ile anaingia wodini anakuta bahasha ya dawa imewekwa pembeni ya kitanda huku mama yake akiwa amelala Anamuuliza mdogo wake mdogo wake anajibu "rafiki yako alikuja hapa akachukua maelezo ya daktari kisha akaenda kununua hizo dawa. Na ametoka hapa muda si mrefu. Kwa furaha kijana anamfuata rafiki yake na kumuuliza "vip ulikuwa wapi? Mbona ulinizimia simu?" Kwa upole rafiki anamshika begani kisha anasema "nisamehe sana rafiki ya...

HAKIM ABDALLAH

Image
HAKIM ABDALLAH shotokan karate player from Tanzania. Started playing shotokan karate in 2013. He gained 1st Dan black belt in December 2016. All this time he has been under the training from Sensei Yahya Mgeni

SHULE ZENYE ADA KUBWA ZAIDI TANZANIA

TOP 10 SHULE ZENYE BEI KUBWA TANZANIA TUSHIRIKISHANE VITU VIZURI 10. Morogoro International School (MIS) Katika Shule ya MIS ada yake kwa mwanafunzi ni kati ya Sh 4.4 Milioni  kwa shule ya Chekechea na Sh 17 milioni kwa elimu ya  Sekondari. Shule hii ni ya gharama kubwa zaidi katika eneo la mkoa wa Morogoro. Shule inatumia mtaala wa Cambridge. 9. International School of Moshi (ISM) ISM ni shule ghali zaidi katika eneo la Moshi. Ada ya kila mwanafunzi kwa mwaka ni kati ya Sh 14.5 Milion kwa elimu ya msingi na Sh 17.2 Milioni  kwa elimu ya Sekondari. Shule inatumia mtaala wa IB. 8. Aga Khan Shule ya Msingi na Sekondari Aga Khan ipo nafasi ya nane kwa Shule za gharama kubwa Tanzania. Ipo katika eneo la Dar es salaam. Mwanafunzi wa ngazi ya msingi,  kila mwaka ada ni  kati ya Sh 7.2 Milioni na Sh 20.4 Milioni kwa ngazi ya sekondari. Aga Khan inatumia mtaala wa IB. 7. Hope of Peace Academy (HOPAC) Hopac ni Shule ya kikristo ya Kimataifa inayopatikana Dar ...