RAFIKI WA KWELI

Ni mida ya saa kumi na moja saa za jioni kijana anampigia simu rafiki yake na kusema "samahani rafiki yangu ninashida na hela, mama yangu anaumwa na hapa nilipo sina pesa ya matibabu.

Rafiki anajibu "usijali!! Nipigie baada ya mechi saivi nipo kucheki game ya simba na yanga

Baada ya mechi anampigia anakuta sim imezimwa
Kama haamini hivi anapiga tena na tena  lakini bado simu haipatikani

Anajaribu kuwatafuta marafiki zake wengine lakini wote wanasema hawana pesa.

Mikono nyuma huku machozi yakimlenga anaamua kurudi hospitalini
Ile anaingia wodini anakuta bahasha ya dawa imewekwa pembeni ya kitanda huku mama yake akiwa amelala

Anamuuliza mdogo wake mdogo wake anajibu "rafiki yako alikuja hapa akachukua maelezo ya daktari kisha akaenda kununua hizo dawa.
Na ametoka hapa muda si mrefu.

Kwa furaha kijana anamfuata rafiki yake na kumuuliza "vip ulikuwa wapi? Mbona ulinizimia simu?"

Kwa upole rafiki anamshika begani kisha anasema "nisamehe sana rafiki yangu sikuwa na pesa hivyo nikaamua kuuza simu yangu kwaajili ya kumnunulia mama yako dawa.

A FRIEND IN NEED IS A FRIEND INDEED.

Mwenyezi Mungu awabariki marafiki kama hawa.

Comments

Popular posts from this blog

SHULE ZENYE ADA KUBWA ZAIDI TANZANIA

STOP SHARING