WANAVYUO KUWENI NA MALENGO
"WANAFUNZI NA WAENDESHAJI VYUO VIKUU JIWEKEENI MALENGO MAKUBWA" Alhaj Dr. Mangochi Wanafunzi wa vyuo vikuu, wahitimu waendeshaji na wamiliki wa vyuo vikuu pamoja na wadau wote wa elimu nchini wametakiwa kuwa na malengo makubwa ili kufikia hatua iliyofikia na nchi nyingine. Akiongea kwenye mahafali ya chuo cha utumishi na chuo kikuu cha Sauti jana mjini Mtwara mkuu wa chuo kikuu cha Mar-wa Dr. Nurdin Mangochi amesema dunia imefika mbali sana na malengo yetu yakiwa madogomadogo dunia inazidi kwenda mbali na kupiga hatua kubwa zaidi huku ikituacha sisi tukiendelea kuwa watazamaji na watumiaji. "Wakati nchi sasa zinadhamira ya kufundisha watu wote kwa kiwaango cha chuo kikuu na kuwa na taasisi nyingi na kufundisha fani zote na kubuni fani nyingi mpya bado sisi tuna vyuo vichache, tunatoa mafunzo kwenye vitivo vichache na wanafunzi wachache zaidi pia tunatumia mbinu za miaka hamsini nyuma." Amesemaa na kuendelea "bado jamii inaona haiwezi kuanzisha vyuo vikuu kila...