NITAOA NIKIFIKA THELATHINI Si kama nataka kufa, kwa haya nitokwambia Ila nofia kujuta, pindi yakikutokea Nogopa nafsi nisuta, mjomba nsipokwambia Nitaoa nikifika thelathini Natambua nia yako, nia unopigania Sikukwacha peke yako, pekee kiteketea Shikamana na wenzako, usia me nakwambia Nitaoa nikifika thelathini. Nataka kupa wosia, li kazi uufanyie Sio uje puuzia, sitajilaumu mie Kidogo hebu sikia, kisha ukazingatie Nitaoa nikifika thelathini. Wangindo mi nawajua, na hasa nawatambua Kidogo kifanikiwa, haraka taka kuoa Mjomba we zingatia, usi harakie ndoa Nitaoa nikifika thelathini. Kama ukipata kazi, tulia kwa kujipanga Usijivishe li vazi, kabla maisha kujenga Tena ipo wazi wazi, kuo...